Monday, December 24, 2012
According to a study by economist Joel Waldfogel, much of what we give each other as gifts is a wasted effort. Of the roughly thirty-eight billion dollars that Americans spent on gifts in a resent Christmas season, Walkfogel estimates that between four billion and thirteen billion dollars is spent on gifts that gave no value to the receiver whatsoever.
Saturday, December 22, 2012
According to Peter Meiksins and Peter Whalley, sociology professors at Cleveland State University and Loyola University, Chicago, respectively, Europeans are more inclined to work part-time because of generous mandated government benefits like pensions, government-subsidized college education, universal health care..
Building Stronger Universities is a partnership between research and higher education institutions are developed, The long-term goal of the initiative is to make the participating institutions stronger in the sense that they:
play an increasing role in
the economic, social and political development of the societies in which
they are located;
function as nodes of
innovation and knowledge production, providing solutions to local/domestic
and global challenges;
produce skilled and
motivated graduates that can contribute to the further development of the
societies and address the challenges
faced.
- Higher education is a dynamo for economic growth, powering the supply of high-level skills and the technological advances for improving productivity and opening up new markets.
- Higher education is a dynamo for economic growth, powering the supply of high-level skills and the technological advances for improving productivity and opening up new markets.
Tuesday, December 18, 2012
STORI YA FAHAMU.
·
Kada asisitiza kulikuwa njama
mbaya Dodoma
·
Amshangaa Hussein Bashe kuzungumza
uongo
Na Mwandishi Maalum
KATIKA hali ambayo baadhi ya wachambuzi wa siasa wanaweza kusema kwamba bado si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, kada mmoja ameendelea kulalamikia hujuma na usaliti, akisema haitoi picha ya uzalendo kwa wanachama wenye nia njema.
Katika mahojiano na FAHAMU, Agustino Oscar Matefu, ambaye pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, alisema amesikitishwa na taarifa za hujuma dhidi ya kura za Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kumhusisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe.
“Nimesikitishwa kuona mwanaCCM mwenzetu Hussein Bashe, akiamua kutumia jukwaa na kunitukana, huku akitoa madai kwamba wahusika wakuu wa hujuma kwenye kikao cha CCM ni pamoja na Waziri Membe,” alisema Matefu.
Matefu alisema kwamba taarifa hizo za Bashe hazikuwa na ukweli bali zililenga kupotosha jamii na hasa wanachama wa CCM, waliokuwa wakitaka kuwafahamu wahusika wakuu wa hujuma hizo.
“Nina lengo ni moja tu la kusahihisha uvumi na taarifa zisizo sahihi zinazoendelea kuzagaa kwenye vyombo vya habari na hata medani za kisiasa tangu nifanye mkutano wangu na wanahabari Dodoma tarehe 9 Novemba, 2012 kuhusu mpango wa baadhi ya wana CCM wenzangu kutaka kumpunguzia kura Mwenyekiti wetu wakati wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi,” alisema Matefu.
Matefu aliongeza kusema kwamba alitoa taarifa dhidi ya wanachama wenzake ndani ya CCM waliokuwa wakitaka kufanya njama na hila kupunguza kura za Mwenyekiti Kikwete.
“Nilipoongea siku ile nilikuwa na akili timamu na sikuwa natania na ndio maana sikuishia tu kutoa taarifa ile kwa vyombo vya habari, bali hata kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ili viweze kufuatilia na ikiwezekana kuchukua hatua,” alisema.
Hata hivyo, kada huyo alisema kinyume na mategemeo yake, akashangaa kuona kada mwenzake, Bashe, anapanda kwenye vilinge vya siasa kuhubiri siasa za kukomoana na kumshambulia kwa matusi ya nguoni.
“Napenda kutumia nafasi hii kuuhakikishia umma wa Watanzania kwamba Mheshimiwa Membe, ahusiki katika kampeni chafu za kumhujumu Mwenyekiti na huhitaji kuwa kibaraka wa mtu kusimamia haki na kuwaepusha viongozi wetu na hila mbaya ya baadhi ya wanasiasa wenzetu ndani ya chama,” alisema Matefu.
Alisema kwa hatua ya kulisemea jambo hilo , amaamini kuwa alitimiza wajibu wake na kwamba ataendelea kusimama katika maneno yake na kuwahakikishia kuwa atapambana na yeyote atakayejaribu kutumiwa kwa nia mbaya dhidi ya serikali na chama cha Mapinduzi.
Aliongeza kusema kwamba kinachomshangaza kuona mtanzania wa kawaida na mzalendo, hasa aliyelelewa CCM anaweza kusimama kwa ujasiri wa kutukana viongozi wa chama tawala na serikali.
Alisema ni kinyume cha misingi ya CCM mtu mzima kusimama kwa ujasiri kutukana viongozi, na kwamba hali hiyo hufanywa na watu wenye upungufu wa akili, mwendawazimu au vijana waliyepoteza mwelekeo, uzalendo na mapenzi mema kwa chama na serikali iliyoko madarakani.
Hata hivyo, Bashe alipotakiwa na FAHAMU kulitolea ufafanuzi suala hilo na hasa kuhusu tuhuma zilizotolewa na Matefu, hakuweza kupatikana, kwani simu yako ya mkononi ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Katika mkutano wa nane wa CCM mjini Dodoma, kulikuwa na tetesi la kundi moja la makada waandamizi ndani ya CCM kuwa na mkakati wa kushinikiza kutenganishwa kwa madaraka ya Rais na ile ya Uenyekiti wa Taifa wa chama.
Lakini hoja hiyo iliyokuwa imeanza kupigiwa debe na baadhi ya wanachama ilipingwa vikali na wazee waasisi wa CCM wakisema ingeweza kukivuruga chama hicho na kutoa mfano wa hali ya mambo ndani ya Chama tawala cha Afrika Kusini (ANC) baada ya kutenganishwa kwa madaraka hayo.
Hata hivyo, wakati waasisi hao wakiwa na misimamo hiyo, na kuonyesha kuwakera walioandaa mkakati huo, ikaibuka hoja ya Mwenyekiti Kikwete kutakiwa kupigiwa kura za maruhani, lakini pia vipeperusi vikaanza kusambaa katika mji wa Dodoma kuonyesha kusisitiza hoja ya kutenganishwa madaraka hayo iendele.
MWISHO.
Subscribe to:
Posts (Atom)